Deuteronomy 30:15-20

15 aTazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo. 16 bNinakuamuru leo kwamba umpende Bwana Mwenyezi Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye Bwana Mwenyezi Mungu wako atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki.

17Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu, 18 cnakutangazia leo hii kwamba hakika utaangamizwa. Hutaishi maisha marefu katika nchi unayovuka Yordani kuiingia na kuimiliki.

19 dLeo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi, 20 ena ili upate kumpenda Bwana Mwenyezi Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa Bwana ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Copyright information for SwhKC